WATUHUMIWA WA KESI YA UGAIDI Wafikishwa Mahakama ya Kisutu leo chini ya Ulinzi Mkali

Ulinzi mkali wa aina yake uliimarishwa leo katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam wakati watuhumiwa 23 wa kesi ya ugaidi ambao ni wafuasi wa Jumuiya ya uamsho na mihadhara ya Kiislamu, wakiongozwa na Kiongozi wao Sheikh Farid Hadi Ahmed walipofikishwa mahakama kwa kujibu tuhuma za ugaidi.
Ulinzi huo ulihusisha vikosi mbali mbali vya Polisi ikiwemo vikosi vya Mbwa,ambapo askari walivaa mavazi maalum huku wakiwa na silaha nzito za kivita wakiwa wametanda katika eneo lote la mahakama kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.
Katika lango kuu la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, magari na watu wote waliokuwa wakiingia eneo hilo walikaguliwa na vifaa maalum huku wale wasiohusika hawakutakiwa kabisa kusogea eneo hilo la mahakama.
Sheikh Farid Hadi na wenzake 23 wanashitakiwa kwa makosa ya kula njama ya kutaka kufanya Ugaidi, kesi ambayo imekuwa na matukio kadhaa ikiwemo washitakiwa kugoma kula, pamoja na kugoma kushuka katika magari kwa madai ya kutaka kesi hiyo itolewe uamuzi haraka kwa sababu watuhumiwa wamekaa muda mrefu mahabusu.
Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa bila kuruhusiwa waandishi wa habari na watu wengine imeahirishwa hadi Julai 30 mwaka huu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo