Siasa tamu, Nape Nnauye achukua fomu za kugombea Ubunge

Baadhi ya vigogo wa serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na waliokuwa baadhi ya wabunge wa majimbo nchini, jana walijikuta wakipigana vikumbo katika ofisi za chama hicho kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania ubunge katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini Oktoba 25, mwaka huu.
 
 Hatua hiyo ilikuja baada ya Chama hicho kutangaza kuanza kutoa fomu hizo jana kwa wanachama wake wanaotaka kuteuliwa na chama hicho kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini kwenye uchaguzi huo utakaovishirikisha vyama vingi vya siasa nchini.
 
Ni baada ya kukamilisha mchakato wa kumpata mgombea wake wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Dk. Ali Mohamed Shein kwa Zanzibar katika vikao vya chama hicho vilivyomalizika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
NAPE ACHUKUA FOMU
Nape  jana alikuwa miongoni mwa wanachama wanane wa CCM waliokabidhiwa fomu za kuwania ubunge katika majimbo matatu ya Wilaya ya Lindi likiwamo la Mtama baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe kabla ya Rais Jakaya kulivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni baada ya wabunge kumaliza kipindi chao cha miaka mitano. Hata hivyo Membe alitangaza hatagombea tena katika jimbo hilo baada ya kutangaza nia yake ya kukiomba chama hicho kumteua kugombea urais Oktoba 25, mwaka huu.
 
Wengine na majimbo hayo kwenye mabano ni  Bakari Said Maguo; Masoud Ally Mikorogo na Ibrahimu Kadhi Ibrahimu (Lindi Mjini), Yusufu Amani;  Adamu Kulagwa na Dk. Alawi Mikidadi (Mchinga).
 
 Makatibu wa CCM Mohamedi Kateva (Wilaya ya Lindi Mjini na Christina Gukwi (Lindi Vijijini) wamethibitisha wanachama hao kuchukua fomu hizo jana. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo