DKT. MAGUFULI NA MH. SULUHU WAPOKELEWA KWA SHANGWE ZANZIBAR LEO

Wananchi na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi CCM wakiwapokea kwa shangwe Mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea mwenza Mh.Samia Suluhu Hassan mapema asubuhi hii mara baada ya kuwasili mjini Unguja -Zanzibar kujitambulisha kwa chama na Wananchi kwa ujumla.
Mgombea urais wa jamhuri ya mungano kupitia chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amewasili Zanzibar kwa kujitambulisha na kupokolewa na mamia ya wanaccm waliojipanga mitaani huku akitamka nafasi yake hiyo haitokani na vita vya panzi.

Mhe Magufuli ambaye amepata tiketi hiyo huko Dodoma awali aliwasili uwanja wa ndege wa Zanzibar akiwa amefutana na mgombea mwenza Mhe Samiha Suluhu Hassan na kupokolewa na wanaccm waliongozwa na makamu wapili wa rais balozi Seif Ali Iddi ambapo badae alipata fursa yakuongea na waandishi wa habari huku akikataa kujibu swali la kuhusu utendaji wa serikali kwa vile muda wake bado ingawa alikanusha kuwa kupata nafasi hiyo haitokani na vita vya panzi ila utaratibu wa CCM ndio uliompa tiketi hiyo.
 
Baadaye msafara huo ulielekea ofisi kuu ya CCM kwa kupitia barabara  kuu ya Michenzani ambapo Mhe Magufuli akiwa na mgombea mwenza walipita barabarani na kusalimaina na wananchi waliojipanga.
 
Wakiwa ofisi kuu ya CCM wagombea hao waliungana na makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni rais wa Zanzibar Dr Ali Sheni ambaye aliwaongoza maamia ya wanaccm na viongozi mbalimbali huku Dr Shein akisema CCM imepata jembe wakuongoza nchi naye kwa upande wake mgombea mwenza Mhe.Samiha Suluhu amesema wakati umefika kwa wanawake kuonyesha ujasiri wao.
 
Mhe Magufuli akiwahutubia wanaccm hao aliwaahkishia kuwa endapo ataupata urais atakuwa ni muadilifu na kuwatumiawanchi wote bila kujali itikadi za vyama.
 
Huu ni ujio wa pili wa viongoi wa CCM wiki iliopita Dr Shein naye aliwasili kutoka Dodoma baada yakupitishwa kugombea urais wa Zanzibar.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo