Katika hali isio ya kawaida shule ya msingi juhudi wilaya Morogoro imefungwa kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kukosa choo ambapo wazazi wamelazimika kuchangishana na kujenga matundu ya vyoo lakini hadi sasa serikali haijafungua shule hiyo huku wanafunzi wakizagaa mitaani kwa zaidi ya miezi miwili bila kusoma.
Wakizungumza kwa jaziba wazazi wananchi wa kijiji cha Mtego wa Simba ilipo shule hiyo wamemlalamikia kuwa baada ya shule kufungwa wamelazimika kuchangishana fedha na kutengeneza matundu ya vyoo 13 lakini hadi sasa shule haijafunguliwa huku walimu wanaonekana wakizagaa mitaani na wakiendelea kupokea mishahara bila kufanya kazi ambapo wazazi hao wametishia kuhamisha watoto wao endapo serikali haitafungua shule hiyo.
Naye afisa elimu wa wilaya ya Morogoro Bw.Donald Pambe akijibu tuhuma za malalamiko ya wazazi amesema ni kwelishule zilifungwa kwa utaratibu kutokana na kukosa matundu ya choo lakini ameahidi kutuma timu yake kufanya ufuatiliaji.