Msanii Recho aongelea skendo ya kutumia dawa za Kulevya

Msanii wa muziki Recho almaarufu kama Recho Upepo ambaye alitamba na nyimbo kama Upepo, Kizunguzungu, amefunguka na kusema kuwa yeye hatumii madawa ya kulevya kama ambavyo watu mtaani wanavyodai.

"Kiukweli mimi situmii madawa ya kulevya hata kidogo, na huwa naumia sana roho napokuwa naambiwa hizi taarifa juu ya kutumia madawa ya kulevya, siijui hata ladha yake ila nadhani watu wanakuwa wakinifananisha, unajua mimi huwa nafananishwa sana na Ray C hivyo labda ndiyo sababu ya hizi taarifa kuwepo mtanii ila kiukweli mimi si mtumiaji wa madawa ya kulevya" amesema Recho 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo