Picha: Dkt John Pombe Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan watua Dar leo, wapokewa kwa shangwe

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiongea na wanahabari mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana huu wakitokea Dodoma na kupokelewa kwa shangwe na umati wa makada wa CCM. 
Mgombea urasi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiambatana na mgombea mwenza Bi Samia Suluhu Hassaan wamepokelewa na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar-es-Salaam na viunga vyake huku mgombe Dkt Magufuli akisema anakerwa na watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu wao.

Dkt Magufuli na mgombe mwenza Bi Samia Suluhu waliwasili uwanja wa ndege wa Dar-es-Salaam majira ya saa saba mchana wakitokea mjni Dodoma na kupokelewa na viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho wa mkoa wa Dar-es- Salaam ambapo walishindwa kujizuia furaha zao na kuanza kuimba nyimbo za kumpongeza kwa kumuita buludoza na kuomba awape takwimu.
 
Mgombea huyo aliwasili katika uwanja wa Mbagala Zakiemu manisipaa ya Temeke jijini Dar-es-Salaam na akiwa katika gari la wazi na kuwasalimia wananchi waliofurika kushuhudia mapokezi hayo, ambapo viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa manisipaa zote za jiji la Dar-es-Salaama bila kujali itikadi zao walimshangilioa kwa furaha na bashasha kubwa.
Akiwasalimia wananchi hao mgombea huyo Dkt John Pombe Joseph Magufuli amewaambia wananchi hao waendelee kumuombea na kuwa atafanya kazi waliyomtuma na kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo, na kusisitiza kuwa yeye ni mpole ila anachukia watendaji wa serikali wazembe wasiotimiza wajibu wao na kuwaacha Wananchi wakiwa na kero mbalimbali bila kuzipatia ufumbuzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo