Wakati zoezi la uandikishaji kwa njia ya BVR likiendelea Dar es salaam…bado kuna maeneo ambayo vurugu za uandikishaji zimeendelea kutokana na vituo kuzidiwa watu.
Hekaheka ya Leo ya kituo cha redio Clouds FM inatokea maeneo ya Mwananyamala ambapo kuna mama mmoja amejikuta akipigwa sana na mume wake hadi kumvua nguo kisa amechelewa kumpikia baada ya kuchelewa kurudi nyumbani akitokea kujiandikisha.
Anasema alimuaga vizuri mumewe lakini alipofika alikuta foleni kubwa..akamaliza saa 9..aliporudi nyumbani mume wake akaanza kumpiga kwa kuwa amemchelewesha kula mchana kisha akamfukuza akiwa na mtoto wake na kuamua kukimbilia kituo cha wanaharakati.
Msikilize hapa…