Na Matukiodaima BLOG
BAADA ya jana kuzomewa na kunusurika kichapo kabla ya kushushwa jukwaani kwa
nguvu kutokana na kubeza kazi kubwa za kimaendeleo zilizofanywa na mbunge Deo
Filikunjombe katika jimbo hilo la Ludewa mtia nia ubunge kupitia chama cha
mapinduzi kepteni mstaafu Jacob Mpangala azidi kulikoroga kwa wananchi baada ya
wananchi wa kata ya Iwela na Luilo kumpinga hadharani kutokana na ahadi yake yakujenga benki ya wananchi Ludewa kila kijiji cha jimbo hilo.
Pamoja na kupinga vikali ahadi hiyo walioiita ni ahadi ya kuwadanganya pia wananchi
hao walimpinga mtia nia huyo kuwa ni muongo kufuatia kauli yake ya kudai kuanzisha
kilimo cha umwagiliaji katika kata ya Luilo na Iwela wakati katika maeneo hayo ni
milima.
Mtia nia huyo ambae anatokea eneo la Manda kando ya ziwa nyasa baada ya kubanwa
juu ya nini amekifanya katika wilaya hiyo ya Ludewa alijikuta akizomewa kwa mara ya
pili na hata wananchi kususa kuendelea kumsikiliza baada ya kudai kuwa yeye ndie
aliyeanzisha kambi ya jeshi Mada wakati katika maelezo yake akidai kuwa alistaafu kazi
ya jeshi mwaka 2008 na kambi hiyo imeanzishwa mwaka huu.
Wananchi hao ambao ni wanachama wa CCM walidai kuwa wamelazimika kuondoka katika
mkutano huo baada ya kumsikiliza mbunge wao Filikunjombe na kuridhishwa na ahadi
zake na kazi alizozifanya ila wamemuona mtia nia huyo anawadanganya kwa kuwapotezea
muda bure kwani wanachoamini wao kazi ya kuwaondoa hofu wananchi wa mwambao
mwa ziwa nyasa juu ya kauli za aliyekuwa rais wa Malawi wakati huo Joyce Banda
aliyekuwa akitishia kutaka kumiliki ziwa hilo lote ilifanywa na mbunge wao ambae
alikuwepo madarakani na mtia nia huyo kwa wakati wa mgogoro huo mwaka jana
hakuwepo kazini .
‘’ Ni kweli ndani ya CCM kuna demokrasia ya kila mwenye sifa kujitokeza kugombea ila
tunachokiona kwa hawa wagombea wawili waliojitokeza kumpinga mbunge wetu
Filikunjombe ni wazi wametumwa na mafisadi kuja kutaka kutuvuruga na mbaya zaidi
hawana jipya la nini watafanya na ndio sababu wanatumia muda mwingi kutudanganya
kwa kuokoteza sera za uongo ……..tunasema hatudanganyiki na hawa wanaokuja wakati wa
uchaguzi wananchi wa Ludewa hawana shida ya kuchagua mbunge mpya nje ya jembe lao
Filikunjombe kwani huyo injinia zephania chaula hii ni mara ya tatu
anagombea ila akikosa huwa haonekani tena hadi mwaka wa uchaguzi tunasema mwaka
huu hatudanganyiki na ili kuwaonyesha kuwa wana Ludewa tupo na jembe letu mwaka
huu tutawachapa kweli’alisema John Haule .
Huku Jane Lukuwi akidai kuwa wana ya uongozi wake wameyaona na kuongeza kuwa
watia nia hao wawili wote katika maelezo yao wanakubali kutumwa kugombea ubunge
na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo prof Raphael Mwalyosi ambae walimuacha baada ya
kushindwa kufanya kazi za kimaendeleo kwa kipindi chote cha miaka mitano hivyo kama
wao walivyojichagulia mbunge bora mwaka 2010 hawana shida ya kuchaguliwa mbunge na
mbunge aliyeachwa kwa kutowatumikia wananchi.
‘’Hawa wagombea wawili tunawashangaa sana wanaposema wametumwa na mbunge prof
Mwalyosi na kutamka hadharani kuwa mbunge wao Filikunjombe atakatwa na vikao vya
juu vya CCM tena bila kujizuia wanadai kuwa juu kuna mjumbe mzito wa vikao vya
maamuzi ambae yupo nyuma yao ….tunaomba kukiomba chama tawala wakitaka kujua
wao wanauamuzi gani juu ya jembe lao Filikunjombe basi waruhusu huyo kigogo wa juu
wa vikao vya maamuzi kupokonya haki yao kwa kukata jina la jembe letu ‘’leo kijiji cha Luilo
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe akijinadi kwa wananchi hao mbali ya
kuwashukuru kwa kuendelea kuonyesha imani kubwa kwake bado alisisitiza kuwa kamwe
hatasinzia bungeni kama walivyofanya baadhi ya wabunge wenzake na kuwa siku zote
ataendelea kupigania maendeleo ya jimbo la Ludewa na kuwa kwa vile bado anaupenda
ubunge na anawapenda wana Ludewa hataacha kuendelea kushirikiana nao kuleta
maendeleo.
Alisema hadi sasa anajivunia maendeleo makubwa ambayo ameyafanya katika jimbo hilo
yakiwemo ya umeme vijjini , uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara , huduma za afya,
kupigania masoko bora ya mazao kwa wakulima, kusomesha yatima 25 kila kata ya
jimbo hilo kwa kila mwaka na maendeleo mengine mengi ambayo sasa yanawavutia
wana Ludewa kutembea kifua mbele tofauti na awali ambapo baadhi yao walikuwa
wakikwepa wilayani hiyo .
‘’Ninatambua wazi kuwa wananchi wangu mnanipenda na mimi nawapenda zaidi hivyo ili tuzidi
kusonga mbele zaidi na kuonyesha kuwa mnanipenda nawaombeni mnipeni kura zote hata kwani baada
ya kazi nzuri ya maendeleo hawa wenzangu wawili wamejitokeza kunisindikiza na ndio maana kila
wanapokwenda wanaishia kupingwa kutokana na haya maelezo yao kuwa wametumwa kunitoa
madarakani ''
Mvuto wa watiania hao wawili umezidi kupungua zaidi kutokana na wananchi ahadi zao ambazo
zinapelekea wananchi kuwapinga kila mkutano hasa ahadi ambayo wananchi wamekuwa wakipinga na
hata kuwazomea ile ya kujenga benki ya wananchi wa Ludewa kila kijiji kwa vijiji vyote zaidi ya 76
pamoja na kuanzisha miji midogo kila kijiji pia kuanzisha kilimo cha umwagiliaji katika vijiji huku
wananchi wakitambua wazi kuwa Jogrofia ya Ludewa ni milima zaidi hivyo kutokana na sera za
watiania hao kuwakwaza wamekuwa wakijikuta wakivunja kanuni za mikutano hiyo ya kutokushangilia
wala kuzomea na kujikuta wakizomewa kila mkutano