Mbunge Wa Karatu kwa Tiketi ya CHADEMA Ajitoa Rasmi Katika Siasa........Atangaza Kurudi Katika Kazi yake ya UCHUNGAJI

Mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji  Israel Natse, amejitoa rasmi katika siasa na kurudia kazi yake ya uchungaji katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini.

Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu ya kiganjani jana, alisema makubaliano yake na chama walimwomba agombee kipindi kimoja tu na sasa anapisha mwingine.

“Mimi ninarudi kwenye kazi yangu ya uchungaji naachana na siasa, huu ndiyo wito wangu nilioitiwa na mungu wa uchungaji,” alisema. 
 
Akizungumza kwa njia ya simu ya kiganjani, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist Lazaro, alisema kwa Jimbo la Karatu waliochukua fomu za kugombea ubunge ni Lazaro  Masai, Fransisca  Duwe, William Kumbalo, Kwamala  Aloyce na Pascal Gutt.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo