Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akipokea kadi za Wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani na kujiunga na CCM,jioni hii katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza,wilayni Chato Mkoani Geita,Mh Magufuli amezoa wanachama wapya waliorudisha kadi zao wapatao zaidi ya 150.
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akipokea kadi za Wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani na kujiunga na CCM,jioni hii katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza,wilayni Chato Mkoani Geita,Mh Magufuli amezoa wanachama wapya waliorudisha kadi zao wapatao zaidi ya 150.Mh Magufuli yuko jimboni kwake Wilayani Chato kuwaaga na kuwashukuru Wananchi wake kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 20 akiwa Mbunge.
MKe wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji huo kwa mapokezi mazuri na makubwa waliyoyapata wilayani humo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara),Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimia wanachama wa CCM pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza wilayani Chato mkoa wa Geita.
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono pia na kuwashukuru Wananchi wake kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 20 akiwa Mbunge wao.
Baadhi ya Wananchi wa mji mdogo wa Muganza,Wilayani Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye viwanja vya mji mdogo wa Muganza jioni ya leo wakishangilia kwa furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao na pia kuwashukuru kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 20 ya Ubunge ndani ya jimbo hilo.
Baadhi ya Wananchi wa mji mdogo wa Muganza,Wilayani Chato na vitongoji vyake wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza jioni ya leo.