Macho yaliyojaa mbubujiko wa Machozi na Nyuso za Huzuni miongoni mwa
wagombea Ni mara baada ya kutangazwa majina mawili yaliyopita kidedea miongoni
mwa majina tisa ya wagombea Ubunge wa Viti maalum wanawake mkoani Iringa
ambao walitumia haki yao ya msingi Katika kugombea nafasi hiyo ambapo baada ya
kura kupigwa na wajumbe wa mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania
mkoani Iringa na Kuwafanya Rose Tweve na Aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum
mkoani kutetea kiti chake kwa kupitishwa kwa mara nyingi kuwaongoza wanawake
hao.
Uchaguzi wa Wabunge wa Viti maalumu ulifanyika ijumaa ya tarehe 24/07/2015
katika ukumbi wa St Dominic Iringa Mjini ambapo jumla ya wajumbe Katika
mkutano huo ni zaidi ya 375 ambao ni wapiga kura halali.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia
ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza alisema kura zilizopigwa zilikuwa
375,zilizoharibika ni 5,ambapo aliwataja wagombea na kura walizopata,alimtaja
Agnesy Nyakunga (4),Farida Ninje(4),Hafsa Mtasiwa(10),Emma
Mwalusamba(14),Esta Chaula(21), Shakira Kiwanga(89), Lediana
Mng’ong’o(162), Ritta Kabati(199), Rose Tweve(240).
Hivyo aliwatangaza washindi kwa mujibu wa katiba ua UWT kuwa wawakirishi wa
wanawake Katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuwa ni Rose Cyplian Tweve na
Mh Ritta Kabati hivyo Katika mchakato huo wa kuwapata wawakilishi hao Mh
Lediana Mng’ong’o ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kutopata kura za
kutosha.
“ndugu wajumbe niwashukuru sana kwa ushirikiano wenu naomba niwatangaze
wawakirishi wenu kuwa ni Ndugu Rose Tweve na Ritta Kabati hivyo sasa wanahitaji
sana wingi wa kura za Urais na Ubunge ndipo wataingia bungeni kwahiyo mnayokazi
ya kufanya kuhakikisha tunakipa ushindi Chama Cha Mapinduzi huko tuendako
Katika uchaguzi ujao”alisema msimamizi
Wakizungumzia mchakato wa uchaguzi huo wagombea walisema wameridhishwa na
mchakato huo pamoja wameridhia ushindi walioupata wagombea wengine na kuahidi
kushirikiana nao kwa kila hali ili kuhakikisha Chama kinapata ushindi wa Kishindo.
Akifunga mkutano huo mwenyekiti wa UWT mama Mwamwindi aliwapongeza
wanawake wote kwa kuonyesha ukomavu wa siasa mara baada ya kwapata viongozi
waliokuwa wakihitajika pia kuwasisitiza kuujenga roho ya Umoja miongoni mwao ili kukipa ushindi Chama.