Kuhusu wananchi kudanganyika na Tisheti na kofia, CHADEMA yatoa somo

Chama cha demokrasia na maendeleo chadema  mkoa wa morogoro kimewakumbusha wananchi wa wa mkoa wa Morogoro  wasidanganyike na zawadi za tisheti kofia badala yake wapime  ahadi  zilizotolewa na viongozi wa vyama vya siasa kama zimetekelekezeka  kabla ya kufanya maamuzi ya kuwapa ridhaa nyingine kuingia madarakani .

Hayo yamelelezwa na mwenyekiti wa uhamasishaji wa chadema kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Morogoro Dododma na Singida Mathew Likwina wakati akihutubia wananchi katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa ndege ambapo amesema wananchi wanakila sababu ya kupima kuona kama huduma waliozoahidiwa wamezipata  kabla ya kufanya maamuzi kwenye sanduku la kupiga kura.
 
Nao watia nia kupitia chama cha demokrasia na maendeleo katika jimbo la Morogoro akiwemo mwanaharakati  Marcus  Urubanus na Steven Daza wamesema sasa wa ni wakati kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro kufunguka na kufanya maamuzi magumu  kuwachagua viongozi wenye uchungu na kero ya tataizo la ajira  na kuhakikisha wanapata ridhaa viongozi watakaosimamia haki na kuhakikisha  kodi za wananchi  zinarudi  kusaidia  wananchi  wenyewe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo