Mtu aliyefahamika kwa jina la Selemani Maporomoko ameuawa kinyama na jirani yake aliyefahamika kwa jina la Mohamed Wajisiku baada ya kuwa na mgogoro wa muda mrefu wa kugombea eneo la shamba lenye heka moja na nusu katika kijiji cha malanje kata ya ntiniko wilaya ya Mtwara vijijini.
Akithibitisha tukio hilo kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa mtwara Henrry Mwaibande amesema marehemu alikutwa na tukio hilo majira ya alfajiri wakati akisafirisha biashara yake ya mbao kwenda mjini kwa baiskeli na ndipo alipoviziwa na jirani yake na kumshambulia kwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili na hatimaye kupoteza maisha.
Tovuti hii imeshuhudia mwili wa marehemu ukiwa umelala pembezoni mwa barabara kuu ya wilaya ya mtwara vijijini na tandaimba huku pembeni kukiwa na baiskeli iliyokuwa imefungwa mbao, ndala za marehemu na kofia, na hawa ni mashuhuda wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa kamanda mtuhumiwa ametoroka na baiskeli yake ilikutwa eneo la tukio hali iliyowapandisha asira wananchi na kuamua kwenda nyumbani kwake na baada ya kumkosa waliamua kuvunja nyumba kubeba kila kitu na hatimaye kuichoma nyumba hiyo moto.
Huku mwenyekiti wa kijiji hicho ismail abdallah akithibitisha kuwapo kwa mgogoro huo wa kugombea shamba.
