Diamond Platnumz amesema kuwa yuko tayari kufanya collabo na msanii yeyote wa Tanzania,
ambaye atakuwa anakidhi vigezo vyake.
Muimbaji huyo wa ‘Nana’ ameyasema hayo baada ya kuulizwa kwanini hafanyi collabo nyingi nawasanii wa Tanzania.
“Mimi sina tatizo as long as nijue hiyo kazi unayotaka kufanya na mimi itafika wapi,” alisema
Diamond kupitia Clouds E.
“umejipanga vipi project yako na umeiandaa vipi, kwasababu sitaki nifanye tu nyimbo mwisho wa
siku halafu iishie tu ndani unaiskiliza wakati natumia muda kukaa kuandika kupoteza muda
studio.“
Aliendelea kwa kujitolea mfano yeye anapofanya collabo na msanii wa nje, lengo kubwa huwa ni
kujitangaza zaidi kule anakotoka msanii anayemshirikisha.
“Na ukiangalia kwa mfano kama nje nakuwa nafanya collabo na wasanii tofauti tofauti kwasababu
inasaidia pia muziki wetu kutanua kiurahisi[…] Lakini haimaanishi kwamba sitaki kufanya collabo
na wasanii wa Tanzania […] yaani unavyokuja kufanya collabo lazima ufanye kuonesha
qualification za kufanya tufanye collabo.”
