CHADEMA Hawataki mchezo, hebu soma hii

Wakati mchakato wa kura za maoni ukiendelea katika vyama mbali mbali ili kutafuta wagombea watakaopeperusha bendera zao katika kinyang’anyiro cha nafasi za uwakilishi wa wananchi katika ubunge, chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoani Tabora kimeapa kuwafukuza uanachama wagombea watakaobainika kutoa hongo ili kujipatia kura za maoni katika nafasi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni katika jimbo jipya la manonga wilayani Igunga na Bukene na Nzega, Bw. Omary Omary wakati akizungumza katika jimbo jipya la Manonga ambapo amesema kuwa, wananchi wameelekeza imani zao katika chama chao kutokana na uadilifu na akijitokeza mtu atakayekiuka maadili chama hakitamvumilia. 
 
Akithibitisha kuwepo na wagombea ambao wametoa rushwa katika kinyang’anyiro hicho katika jimbo la Igunga mashariki, katibu wa Chadema wilaya ya Igunga Bw Athumani Ndagwemeleye amesema kuwa, tayari wamepeleka taarifa kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ili kudhibiti hali hiyo. 
 
Katika uchaguzi wa kura za maoni jimbo jipya la Manonga wilayani humo, uliotanguliwa na dua na sala, kulikokuwa na wagombea watano, ambapo ameongoza Ally Nguzo mwenye shahada mbili za fedha, uongozi, na utawala kwa kura 247 kati ya 289 zilizopigwa, huku nafasi ya viti maalumu Chadema jimbo la Manonga ikichukuliwa na Rucr Samweli mwenye shahada ya elimu maalumu akiibuka mshindi kwa kura 67 kati ya kura 73 zilizopigwa. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo