Askari polisi apata ajali ya kugongwa na bodaboda Morogoro

Afande Mage akigaragara kwenye lami kugongwa na bodaboda.

ASKARI wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (F.F.U) mkoani Morogoro aliyefahamika kwa jina moja la Mage amevunjika mguu na kupoteza fahamu kwa muda baada ya pikipiki aliyopanda kugongana uso kwa uso na bodaboda eneo la Mji Mpya mbele ya kituo cha polisi majuzi.

Afande Mage ambaye alivunjika mguu na mfupa kutoka nje, alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kuendelea na matibabu.

Dereva wa pikipiki aliyokuwa amepanda Afande Mage ambaye pia ni askari polisi aliyefahamika kwa jina moja la Shaibu, hakuumia sehemu yeyote ya mwili wake wakati huo dereva wa bodaboda waliyegongana naye ambaye jina lake halikufahamika aliumia vibaya sehemu ya kichwa za kupoteza fahamu.

Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda wa tukio hilo Siasa Said alisema;

"Hawa maaskari walikuwa wakitokea mjini wakiwa mwendo wa kawaida, huyu kijana wa bodaboda alikuwa akitoka Mwembesongo na alipofika Kituo cha Polisi Mji Mpya akiwa mwendo kasi alijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na kugongana uso kwa uso na pikipiki ya maafande hawa.

Afande Mage alivunjika mguu huku Afande Shaibu akinusurika baada ya kuwahi kuruka alipoiona ajali hiyo" alisema shuhuda huyo.
PICHA/STORI: Na Dunstan Shekidele - GPL, Morogoro


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo