Akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi katika viwanja vya Mwananchi Squer katika mji mdogo wa Urambo mwenyekiti wa UKAWA Ibrahimu Lipumba amesema kuwa, kama UKAWA utaamua kumpitisha mgombea mwingine atakuwa tayari kumpigia debe mteule wa UKAWA, lakini malengo yake ya kutaka kugombea urais, ni kutafuta haki ya wananchi ambayo imepotea.
Aidha katika hatua nyingine Mhe Prof Ibrahimu Lipumba amewataka watanzania kutambua kwa changamoto ambazo zinawakabili zikiwa ni upatikanaji wa haki za kijamii, zitaondolewa na rais ambaye atatoka nje ya chama cha mapinduzi na si vinginevyo, na kama hawatachagua rais kutoka nje ya CCM wajue hali ngumu ya maisha itaendelea kuwakabili kutokana na kutokuwepo na haki.