Mwanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema jimbo la ilala Bwana MUSLIM HASSANAL ametangaza rasmi nia yake ya kumng'oa katika kiti cha Ubunge mbunge wa jimbo la ilala mh MUSA ZUNGU katika uchaguzi ujao mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo ameyasema Jijini Dar es salaam wakati akirudisha Fomu ya kugombea ubunge katika jimbo hilo la ilala tukio lililofanyika katika ofisi za kanda za chama hicho zilizopo kinondoni Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kurejesha Fomu hiyo Bwana MUSLIM amesema kuwa lengo lake ni kuhakikisha kuwa Jimbo la ilala linarudi katika hadhi yake ya kuwa jimbo la mfano katika majimbo yote ya Dar es salaam ukizingatia kuwa jimbo hilo ndilo linalobeba Jina la Dar es salaam kwa kuwa na ofisi mbalimbali na kubwa za serikali.
“Ukizungumzia uchafu Dar es salaam lazima uitaje ilala,ukigusia ubovu wa miundombinu lazima uitaje ilala,ukitaja wananchi kuishi kwa hali duni lazima uitaje ilala,sasa sisi kama chama tumeamua kuhakikisha kuwa hali hii inafutika na tutalirejesha jimbo la ILALA mikononi mwetu kama ukawa watanipa nafasi ya kugombea katika jimbo hilo”alisema mtia nia huyo anayeonekana kujiamini sana.
Ameongeza kuwa ukimtizama unawezaa kudhani yeye sio mtanzania ila kwa ufupi yeye ni mzaliwa wa Tanzania na maisha yake yote amekulia kariakoo,hivyo anajua matatizo ya wananchi wa ilala kwa ujumla,na amejipanga kuhakikisha kuwa anashirikiana na chama chake kwa kupitia ukawa kuwasaidia wananchi hao.
Bwana MUSLIM HASSANAL aliwahi kugombea ubunge katika jimbo la kigoma kaskazini uchaguzi uliopita lakini hakufanikiwa kupita ambapo DAVID KAFULILA wa NCCR-MAGEUZI alishinda, ambapo akizunguzimzia hilo amesema kuwa kigoma ndipo walipo babu zake na ndio maana aliwahi kugombea huko lakini kwa sasa anadhani ni muda wa kumuunga mkono KAFULILA kwani bado anastahili kuongoza jimbo hilo .