Akinamama wawili walioolewa na mme mmoja Bw, Shingu Mashigina, wamekufa kwa wakati mmoja,ambapo mmoja akimpiga mwenzake na Mchi Kichwani na kufa papo hapo,na kisha yeye aliyefanya mauaji, kujinyonga kwa kutumia kanga katika nyumba hiyo hiyo huko katika kijiji cha Tura wilayani Uyui Mkoani Tabora.
Akithibitisha mauaji hayo mara baada ya kutoka katika mazishi ya akinamama hao mtendaji wa kijiji Bw. Masabo Williamu amewataja marehemu kwa majina ya Mindi Salmu (18) mke mdogo aliyeuawa, na Mwenda Kulwa (30),aliyejinyonga baada ya kufanya mauaji ambapo chanzo cha mauaji hakikufahamika mara moja.
Kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ya kutisha huku akiitaka jamii kulaani kitendo hicho cha kinyama kilichofanywa na mama huyo kisha kujinyonga.
