KWA KIJANA YEYOTE HII ISIKUPITE MAANA INAKUHUSU SANA NA ITAKUSAIDIA


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu JUMA KHATIBU CHUM
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu JUMA KHATIBU CHUM amewashauri vijana wa wilaya ya KILOMBERO mkoani MOROGORO kujiepusha na vishawishi vya fedha na itikadi za kiimani zinazoweza kuwaingiza katika vitendo vya uhalifu.

CHUM ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Wakazi wa MLIMBA wilayani KILOMBERO mara baada ya Mwenge wa Uhuru kupitia miradi 9 ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Milioni 850 Nukta 9.

Ukiwa wilayani ULANGA, Mwenge wa Uhuru umetembelea miradi 6 ya maendeleo, yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni Moja.

Miradi iliyopitiwa na mwenge wa Uhuru katika wilaya za ULANGA na KILOMBERO ni pamoja na ile ya ujenzi wa vituo vya afya, maji, maabara za shule, ujenzi wa kituo cha polisi na ile ya mazingira.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo