UTATA MPYA PAMBANO LA MAYWEATHER, PACQUIAO

Karatasi ya matokeo ya majaji watatu Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti zinavyoonyesha na picha inawaonyesha mabondia hao katika kona zao, Floyd Mayweather ya bluu (kushoto) na Manny Pacquiao nyekundu (kulia).

Floyd Mayweather akiwa amekaa kona nyenye rangi blue.
Pacquiao akiwa amekaa kona yenye rangi nyekundu.
UTATA umeibuka kutoka Pambano la Karne baina ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililofanyika juzi ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas, Marekani.
Karatasi ya kuandika matokeo raundi kwa raundi ya majaji wote watatu, Glenn Feldman, Burt Clements na Dave Moretti inaonyesha bondia aliyekuwa kona nyekundu, Pacquiao ndiye aliyeshinda pambano, wakati mtangazaji 'MC' wa pambano akamtangaza bondia wa kona ya bluu, Mayweather ndiye mshindi.
Inaonekana kama majaji walijichanganya katika kutumia karatasi hizo na pointi za Mmarekani, Mayweather 'Mtu Pesa' wakizihamishia kwa Mfilipino, Pacquiao, lakini kwa nini iwe kwa majaji wote watatu?
Hii inazidi kuzua shaka kwamba inawezekana Mayweather alipewa ushindi kimakosa bali kwa mujibu wa karatasi za majaji mshindi ni Pac Man aliyekuwa anatokea kona nyekundu.
(CHANZO: DAILY MAILY)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo