MTOTO wa nne wa Mwalimu J.K Nyerere, John Nyerere amefariki dunia juzi akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.
Marehemu John alizaliwa mwaka 1957 jijini Dar es Salaam na enzi za uhai wake alikuwa kapteni wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita.
Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia ni kwamba marehemu amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu na kisukari kwa muda mrefu.
Enzi za uhai wake John alishiriki vita ya kumng'oa Nduli Idd Amini nchini Uganda.
Mungu ailaze roho ya marehemu John mahali pema peponi. AMENI