SIMBA WALIOTOROKA HIFADHI YA SELOU WASABABISHA MAKUBWA HUKO SONGEA

Wananchi katika kijiji cha MATEMANGA wilayani tunduru mkoani RUVUMA wanaishi kwa hofu na kulazimika kutotembea usiku wakihofia kuliwa na simba wanaosumbua katika kijiji hicho  wakidaiwa kutoroka katika hifadhi ya taifa ya  SELOU  ambapo  mpaka sasa wameshakula mbuzi  zaidi ya ishirini.

Wamesema simba hao wanaodaiwa kuwa watatu na wazee ambao ina daiwa wametoroka porini baada ya kushindwa kuwinda kutokana na uzee ambapo wameshakula mbuzi zaidi ya ishirini kijijini hapo  wamekuwa wakisumbua katika kijiji hicho nyakati za usiku  na kuwafanya waishi kwa hofu  wakihofia kuliwa na simba hao.
 
Mhifadhi wa wanyamapori katika wilaya ya tunduru Bw.Charles Shawa  anasema kuwa msako mkali wa kusaka simba unaendelea huku akisema ni simba mmoja  tu ndiye  anayesumbua  kijijini hapo.
 
Mkuu wa wilaya ya tunduru Bw.Chande Bakary Nalicho anasema nguvu zimeongezwa katika msako wa simba  ambapo kuna askari wanyamapori sita katika  msako wa simba.
 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo