Serikali yatakiwa kutoa majibu ya ni lini itawafidia wananchi walioathiriwa na operesheni tokomeza

Serikali imetakiwa kutoa majibu ya ni lini itawafidia wananchi walioathiriwa na operesheni tokomeza wakiwemo waliochomewa nyumba zao huku wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam wakitishia kukwamisha bajeti ya wizara ya miundombinu kutokana na kushindwa kumaliza tatizo la foleni.

Wakichangia bajeti ya ofisi ya waziri mkuu bungeni mjini Dodoma wabunge hao akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya bunge iliyochunguza sakata la operesheni tokomeza Mh James Lembeli wamesema baada ya ripoti kubaini mapungufu yaliyojitokeza katika operesheni hiyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha inawalipa fidia wananchi ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba.
 
Baadhi ya wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na mwenyekiti wao Mh Abasi Mtemvu wamedai kuwa hawatashiriki kupitisha bajeti ya wizara ya miundombinu kutokana na ahadi za muda mrefu ambazo waziri wake amekuwa akizitoa lakini tatizo bado linazidi kuongezeka hali inayokwamisha kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi.
 
Hata hivyo mjadala huo umekuwa na mihemko mikali ya wabunge ambao asimilia kubwa wameitaka serikali kutoa majibu ya kwa nini bunge linatumia muda mwingi kuidhinisha bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo lakini mwaka wa fedha unakwisha fedha hizo hazijafika na zikipelekwa ni pungufu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo