Baraza la mawaziri la nchi za jumiya ya Afrika mashariki limesema hali ya amani katika nchi ya burundi bado ni tete na kamati hiyo itakutana siku ya jumatatu wiki ijayo ili kufanya tathimini ya hali itakavyoendelea kuwa nchini Burundi na nini kifanyike kwani mpaka sasa haijajulikana kuwa ni nani anayeongoza nchi hiyo kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Piere Nkurunziza na wanajeshi waliofanya mapinduzi.
Mwenyekiti wa mawaziri hao ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Tanzania Bernard Membe amesema kwa hali ilivyo hivi sasa nchini burundi zinahitajika jitihada za ziada kwa kila mpenda maendeleo ili kuweza kunusuru vurugu zinazoendelea nchini humo.
Kuhusu mahali alipo Rais Piere Nkurunziza waziri membe amekataa kutaja mahali alipo ingawa uchunguzi umebaini kuwa usiku wa kuamkia leo Rais huyo wa Burundi alilala katika moja ya hotel kubwa za kitalii zilizopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
chanzo:itv