Baada ya hapo kwanza kulikua na taarifa kwenye mitandao mbalimbali kwamba Paul Makonda hakuhusika kumaliza mgogoro huo bali Mwenyekiti Freeman Mbowe.
‘Swala la mgomo wa madereva limekua na athari nyingi na tofauti kwa taifa na tangu mgomo umeanza jana watu mbalimbali wameathirika na upande wa pili bado ni ukweli tu kwamba hata madereva madai yao yana msingi na yanastahili kutatuliwa, kamati kuu ilinishauri nikaweze kuona naweza kuwa wa msaada gani’
‘Aliyefanya mazungumzo hasa rasmi na Madereva alikua ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda na nilipofika nilimkuta akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa madereva na kimsingi walikua walishaafikiana, nilichojaribu kukizungumza ni kuunga tu mkono kwasababu sikuona jambo baya lililofanyika na kuwatia moyo kwa upande huo’