mzee mmoja ambae aliwapiga risasi watu wawili na kuwajeruhi.. watu hawakupendezwa na kitendo hicho, wanasema sio mara ya kwanza mzee huyo kutishia watu risasi.
Baadhi ya watu waliona wafanye maamuzi magumu, wakavamia nyumba ya mzee huyo na kuichoma gari yake moto, wengine walitaka kuichoma na nyumba yake pia… ilibidi kikosi cha Askari kufika na kutumia mabomu ya machozi pamoja na kupiga risasi hewani ili kumuokoa mzee huyo.
Kwa sasa mzee huyo anashikiliwa na Polisi.. Mashuhuda wamesema kisa cha mzee kuwapiga risasi vijana hao ni ishu ya kutopenda kelele wala hataki kelele jirani na nyumba yake.
Watu wengine waliingia mpaka ndani na kuiba vitu pamoja na kufanya uharibifu mkubwa.. Hata baada ya Askari kufika kumuokoa bado watu waliendelea kushambulia ili wamkamate mzee huyo, Polisi ikabidi watumie mabomu ya machozi pamoja na kupiga risasi hewani ili kumuokoa.