MUME AAMUA KUMUACHIA PADRI MKEWE ILI AMUOE

MWANAMUME ambaye ni baba wa watoto wawili ameenda katika Mahakama Kuu mjini Nyeri akitaka ruhusa ya kumpa talaka mkewe kwa madai ya kujihusisha kimapenzi na padri wa kanisa la Katoliki.
Mwanaume huyo amemshtaki Padri Evaristus Rubua Maranga wa kanisa lililoko eneo la Tetu, Kaunti ya Nyeri, kwa kujihusisha na mkewe waliyedumu naye miaka 22 huku akidai zaidi kuwa padri huyo amekuwa akimshawishi mkewe aondoke nyumbani kwake na kuanza kuishi peke yake  ili waendeleze uhusiano wao huo.

Kulingana na hati ambazo amezipeleka kortini, mlalamishi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe analalama kuwa mkewe Bi Beatrice Wairimu amekuwa akifanya ukware na padri huyo kwa muda mrefu na hata kutumia pesa za familia vibaya kwa kumpa padri huyo bila kumjulisha.
Analalamika pia kuwa mkewe amekuwa akimchapa, kumtusi na kumkejeli huku akimletea aibu kijijini kwa  sababu ya tabia zake za uzinzi.
Anasema kilichomuudhi zaidi ni kuwa mkewe anafanya  uzinifu huo na padri wa kanisa lao wanaloenda kuabudu kama familia.
Wawili hao walioana mnamo 1993 kwa mila za kitamaduni za Wakikuyu na amekuwa wakiishi  pamoja kama mume na mke hadi Januari 30, 2013 wakati Bi Wairimu alipoamua kutoka  nyumbani kwao   kijiji cha King’ong’o, Nyeri na kwenda kutafuta makazi yake ya kibinafsi, akimuacha yeye peke yake.
Mwanamume huyo pia anadai kuwa mkewe alienda na watoto wao wawili  bila ruhusa yake akiwemo mvulana wao  ambaye bado hajatimu umri wa miaka 18.
Mabadiliko ya kitabia
Anadai kuwa walipokuwa wakiishi na mkewe, alianza kuona mabadiliko ya kitabia na baada ya kufanya uchunguzi wake, aligundua kuwa alikuwa akijihusisha kimapenzi na padri huyo ambaye pia ndiye anayeongoza ibada kwenye kanisa lao.
Analalama pia kuwa hata baada ya kutafuta  usaidizi kutoka kwa viongozi na mapadri wengine wa kanisa hilo, hakuna  juhudi zozote wala uchunguzi wowote uliofanywa na  kanisa hilo kubainisha  iwapo kuna  ukweli katika malalamishi hayo na ndipo akaamua kutafuta usaidizi kortini.
Padri Maranga ndiye padri mkuu ambaye anasimamia kanisa la Tetu.
Amepewa majukumu tofauti ikiwemo kuongoza ibada na kuendeleza shughuli za kanisa na kuwasimamia mapadri wengine.
Mume huyo anataka apewe ulezi wa mvulana wao ambaye bado hajatimu umri wa kijisimamia na pia mali ya familia igawanywe kati yao na watoto wao wawili.
Anataka pia Padri Maranga na Mkewe Bi Wairimu kuangizwa Kumlipa gharama  ya huzuni na mateso ambayo amekuwa akipitia  kwa kusababisha  ndoa yake na mkewe kuharibika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo