Kenya wamtaka Rais Kikwete kuingilia kati mgogoro Wa Burundi


Wananchi  nchini Kenya wamemtaka mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye ni Rais wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete kuingilia kati mgogoro wa Burundi uliopelekea wanachi zaidi  ya kumi kufariki dunia na wengine kukimbilia nchini Tanzania.
 
Wakizungumza katika maandamano hivi karibuni  ya kumpinga Rais Nkurunziza  kugombea tena urais raia hao wa Kenya wamemshinikiza Rais Nkurunziza kusitisha mpango wake wa kugombea tena muhula mwingine ili kuzuia machafuko yanayoendelea nchini Burundi hivisasa.
 
Hadi sasa takribani watu 18 wamefariki dunia kutokana na machafuko hayo huku mahakama ya kikatiba ya nchi ikitangaza kumruhusu rais huyo kuendelea kugombea kwa muhula wa tatu suala linalodaiwa kuwa kinyume na Katiba ya nchi hiyo.
 
Aidha, Rais Pierre Nkurunziza amewatangazia wananchi kwamba endapo atachaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo huo utakuwa muhula wake wa mwisho.
 
Kwa upande mwingine Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ameitisha mkutano na wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam siku ya Jumatano mei 13 kujadili mgogoro huo pamoja na Tanzania kutoa msimamo wake dhidi ya Mgogoro huo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo