DKT REGINALD MENGI AFANYA "KWELI" KWA WASICHANA HAWA

Jitihada za maksudi zinahitajika katika kutatua  changamoto za utoaji wa elimu nchini,  kwa vile elimu bora ni msingi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti mtendaji wa IPP Dr.Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi zawadi kwa wananfunzi 12 wa shule ya sekondari ya wasichana Kisutu waliofaulu kwa daraja la kwanza katika mtihani wa taifa  mwaka jana, ambapo kila mwanafunzi alimzawadia  shilingi milioni moja, kama alivyowaahidi wakati wa mahafali yao.
 
Dr.Mengi ambaye licha ya kuwazawadia wanafunzi hao, pia alikabidhi kwa shule hiyo mashine ya kisasa cha kuchapa, seti nne za luninga na mashine ya kutoa kopi, pamoja na kumlipa mshahara mwalimu mstaafu anayefundisha somo la maarifa ya nyumbani,amewataka wazazi kutambua kuwa jukumu la kuwalea na kuwasomesha watoto ni lao wenyewe, hata kama serikali inasaidia.
 
Mapema katika risala yao mkuu wa shule hiyo Bi.Monica Saria, na mwakilishi wa wazazi katika hafla hiyo Bi.Mary Kisaka wamemshukuru Dr.Mengi kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa mahafali ya mwaka jana na kusisitiza kuwa shule ya sekondari Kisutu imekuwa ikifanya  vizuri katika mitihani ya taifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo