Chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema kimefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Kawe jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzindua rasmi mpango uitwao FTP 200 uliolenga kuhakikisha kila kata kinakuwa na walinzi 200 wa chama hicho.
Akizungumza katika uzinduzi huo mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema moja kati ya mambo ya msingi ambayo kwa sasa yanatakiwa kufanyika ni tume ya taifa ya uchaguzi kuhakikisha zoezi la uandikishaji wapiga kura linafanyika kikamilifu la sivyo watabeba mzigo wa lawama.