Wenyeviti walalamikia zoezi la uandikishwaji wa daftari la wapiga kura kwa kutumia mashine mpya za BVR MTWARA

Wenyeviti wa serikali za  mitaa katika kata ya mikindani manispaa ya Mtwara wamelalamikia manispaa kwa kushindwa kuwapa taarifa mapema kuhusu  zoezi  la uandikishwaji wa daftari la wapiga kura kwa kutumia mashine mpya za bvr na badala yake wamepata taarifa za kukurupushwa hali iliyosababisha wananchi kujitokeza wachache katika vituo vya kujiandikisha.

Wenyeviti wa serikali za  mitaa katika kata ya mikindani manispaa ya Mtwara wamelalamikia manispaa kwa kushindwa kuwapa taarifa mapema kuhusu kuaza kwa zoezi  la uandikishwaji kweye daftari la kudumu la  wapiga kura  hali iliyosababisha wanachi wachache kujitokeza katika vituo vya  kujiandikisha.
 
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wenyeviti hao wamesema zoezi hilo ni nyeti hivyo wananchi wangepaswa kupata taarifa mapema ikiwemo manispaa kutumia magari ya matangazo kipita mitaa mbalimbali ya kata hizo.
 
Kwa upande wao waendeshaji wa zoezi hilo wamesema ugumu wa kazi unatokana na ugeni wa matumizi ya mashine za BVR vinginevyo zoezi linakwenda vizuri.
 
Hata hivyo blog hii imeshuhudia katika baadhi ya vituo wananchi wakiwa wachache huku baadhi ya watendaji wa kata hizo wakidai ni siku ya kwanza hivyo muitikio bado ni mdogo na wanaendelea na uhamasishaji, katika kata za mikindani, ufukoni na Mitengo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo