Akizungumza na waombolezaji nyumbani kwa marehemu Kola Hill mkoani Morogoro Rais Kikwete amesema serikali imepoteza kiongozi muhimu aliekuwa mchapakazi ambapo amewataka ndugu na wanafamilia kuwa na moyo wa uvumilivu hasa katika wakati huu mgumu wa kuomboleza kifo cha ndugu yao.
Akitoa salamu kwa niaba ya mkuu wa majeshi majeshi Device Mwamunyange Meja Jenerali Nerali Salum Kijuu amesema marehemu alilitumikia jeshi la wananchi JWTZ kwa uadilifu na uaminifu huku mwenykiti wa wakuu wa wilaya nchini Jason Msome umoja wa wakuu wa wilaya wamestusha na kifo hicho ambapo wameeleza maerhemu alifanya kazi zake kwa ushirikiano wa karibu na wenzake hadi umauti ulipo mkuta.
Kwa upande wake ndugu wa marehemu wameshukuru serikali kwa jitihada za kumuuguza marehemu na kuiomba serikali kuendelea kuwa karibu na familia ya marehemu katika masuala mbalimbali hasa katika wakati huu mgumu wa maombolezo huku askofu mkuu wa jimbo la morogoro Telesphol Mkude amewataka watanzania kufanya matendo yanayompendeza mwenyezimungu kwani hapa duniani tutaondoka na uzima wa milele upo mbinguni.
Marehemu benedict kitenga amefariki april 20 katika hospitali ya taifa ya muhimbili na kuzikwa pril 23 katika makaburi ya kola mjini morogoro ambapo mazishi yake yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali akiwemo waziri mkuu mizengo pinda ,waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa hawa ghasia na waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi selina kombani wakumuu wa mikoa na wakuu w awilaya .