MASHABIKI WA SIMBA UKAWA WAPATA AJALI,YADAIWA WATU 7 WAMEPOTEZA MAISHA


kikundi cha ushangiliaji cha tawi la Simba la Mpira na Maendeleo maarufu kwa jina la Simba Ukawa  wamepata ajali  iliyotokea leo mjini Morogoro wakielekea mjini Shinyanga kuisapoti timu yao inayocheza mechi ya ligi kuu kesho dhidi ya Kagera Sugar.

Taarifa mpya na za uhakika zinasema watu watano (7) akiwemo kiongozi wa Simba Ukawa, Mohammed Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ wamefariki dunia na watu 15 wapo mahututi.

Ajali hiyo imetokea eneo la Mvomero ikihusisha basi dogo aina ya Toyota Costa lililopinduka na kuacha njia. Polisi bado hawajatoa tamko rasmi.


Waliotangulia mbele ya haki mpaka sasa ni:
Waluya, Rehema, Ali Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ Wabi na dereva wa gari Abdallah Fundi.maandishi picha  na Shafih dauda.com 



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo