Hakimu wa kesi ya mauaji ya Dk. Mvungi ajitoa



Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Waliarwande Lema, amejitoa kusikiliza kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi, inayowakabili washtakiwa 11.
 
Tukio hilo lilitokea juzi, baada ya washtakiwa hao 11 kumuomba Hakimu Lema ajitoe kuisikiliza kesi yao ili iweze kupangwa kwa hakimu mwingine ambaye wao wanaona atawatendea haki.
 
Kutokana na ombi hilo, Hakimu Lema alijitoa na kuiahirisha kesi hiyo ambayo upelelezi wake hadi sasa bado haujakamilika na itatajwa tena AprilI 20, 2015, itakapopangwa mbele ya Hakimu mwingine.
 
Mawakili wa Serikali, Ofmad Mtenga na Diana Lukondo walidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na waliomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuitaja.
 
Miongoni mwa washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Chibago Magozi (32), John Mayunga (56), Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Zacharia Msese (33), Msungwa Matonya (30), Ahmad Kitabu (30).
 
Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa mnamo Novemba 3, mwaka 2013, walifanya kosa la mauaji kinyume cha kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo