Wachezaji waliotemeana mate uwanjani waadhibiwa na shirikisho la soka la England

slapPamoja na kukataa kwamba hakumtemea mate mshambuliaji wa New Castle Papis Cisse, beki wa Man United, Jonny Evans amefungiwa mechi sita na  Shirikisho la soka England FA.

Naye Papis Cisse amefungiwa michezo saba na Shirikisho hilo.

FA imetoa adhabu hiyo baada uya kuthibitisha kupitia mkanda wa video hiyo katika mchezo uliochezwa jumatano iliyopita katika uwanja wa St. James Park ambapo Man U waliibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililofungwa na Ashley Young.
evance
Adhabu hiyo itamfanya beki huyo kukosa mchezo wa robo fainali dhidi ya Arsenal siku ya jumatatu kwmenye uwanja wa Old Tranford na michezo mingine atakayoikosa ni ile dhidi ya Tottenham, Liverpool, Aston Villa, Manchester City, na Chelsea.

Kwa upande wa Cisse atakosa michezo dhidi ya Everton, Arsenal, Sunderland, Liverpool, Tottenham,Swansea na Leicester


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo