Siku za mwizi ni arobaini na ikifika arobaini za mwizi anaweza kujikuta kwenye kitanzi kwa njia ambayo hata mwenyewe haamini…
Hii story inatokea Newport, South Wales, jamaa mmoja amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuingia kwenye nyumba moja kwa lengo la kufanya uhalifu japo hakufanikiwa kukamilisha lengo lililomuingiza kwenye nyumba hiyo.
Matthew Waters
alikutwa kwenye chumba cha spare akiwa amelala kwenye kitanda kilichopo
kwenye chumba hicho huku pembeni yake kukiwa na kopo tupu la Ice Cream ambayo inaonekana aliilamba kabla ya kupitiwa na usingizi.
Matthew
aliamka kwa mshtuko baada ya mwenye nyumba hiyo Julie James aliporudi
kutoka kazini na kufungua mlango wa chumba hicho ambacho ana kawaida
kukikagua kila mara akirudi toka kazini.
Baada ya kushtuka, Matthew
alikimbia lakini alikamatwa baada ya sura yake kuonekana kwenye camera
za CCTV, Mahakama ilimkuta na hatia baada ya mpelelezi wa makosa ya
jinai kugundua kuwa amekuwa akiishi kwa kuvamia nyumba za watu na
kuhukumiwa kifungo cha miezi nane jela na kumlipa Julie paundi 100 (sawa na Tshs 270,000/-)