SAFARI YA NDEGE YASITISHWA GHAFLA KISA CHOO....!!!!

Runway
Ni kawaida kusikia kwamba ndege imeahirisha safari ama imekatisha safari kutokana na hitilafu ama dharura, ishu kama ya hali ya hewa ikiwa mbaya haishauriwi kuiacha ndege iendelee na safari hiyo.
Dharura iliyoikuta ndege ya shirika la ndege la British Airways na kulazimika kukatisha safari kutokana na harufu mbaya iliyokuwa ikitokea ndani ya choo hii ni story ambayo iko kitofauti kidogo.
Ndege hiyo ilikuwa imetoka Heathrow Uingereza kuelekea Dubai safari ambayo kwa kawaida huchukua kama saa saba.
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo Abhishek Sachdev, aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa walilazimika kurudi kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow kutokana na tatizo la choo cha ndege hiyo kutoa harufu mbaya.
Abiria huyo alionekana kukasirishwa na kitendo cha safari yao kuahirishwa na kulazimika kurudi Uwanja huo wa ndege ambapo walikaa kwa saa 15 mpaka ilipopatikana ndege nyingine ya kuwasafirisha abiria hao kwenda Dubai.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo