P-Square wanaweza kumtafuta Joti siku yoyote kuanzia mwaka huu.
Hiyo ni baada ya mmoja wa mapacha hao maarufu zaidi Afrika, Paul
Okoye kupost kipande kifupi cha Joti akicheza wimbo wa Koffie Olomide
kwa style iliyomvutia.
Paul ameipata video hiyo kutoka kwenye akaunti ya Instagram iitwayo ‘Nigeriagirlskillingit’.
“Hahahahahaha i can’t wait for psquare to start dancing like this,”
ameandika Paul na kuambatisha na emoji zinazocheka hadi machozi.