MTUHUMIWA HUYU HAPA ATOROKA MAHAKAMANI, ASKARI WALAZIMIKA KUMPIGA RISASI

DSC00660
Mwezi December 2014 kulikuwa na story ya mtuhumiwa mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijaribu kutoroka Mahakama ya Kisutu kwa kuruka ukuta wa Mahakama hiyo, story kutoka Kenya leo inafanana na hii.. inahusu mtuhumiwa mmoja kufanya jaribio la kutoroka kutoka Mahakama ya Machakos.
DSC00659
Mtuhumiwa huyo alijaribu kutoroka lakini askari wakampiga risasi mkononi na mguuni akiwa juu ya ukuta, majeraha hayo yalimfanya ashindwe kukimbia, akakamatwa.
DSC00664
Mahabusu huyo alifikishwa Mahakamani kwa kosa la kufanya vurugu baada ya kulewa na hukumu yake ilikuwa alipe faini ya Kshs 200, jaribio lake la kutoroka limefanya awe na kesi nyingine mpya kutokana na kufanya kosa hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo