Emily Nyondo ndio jina la mwanamke huyo toka Zimbabwe, siku ambayo aliona ajihakikishie ukweli alimfuata mume wake ambaye ni Oscar Nyondo nyuma nyuma mpaka kwenye nyumba ya msichana mmoja, mwanaume huyo akaingia ndani halafu akafunga mlango.
Emily hakuridhika, akasogea karibu zaidi mpaka dirishani na kuchungulia ndani ili aone kila kinachoendelea.
Oscar alikuwa kitandani na msichana Mamsie, Emily aliwaangalia na kushindwa kuvumilia kuuangalia usaliti wa mumewe, akaamua kuondoka na kurudi nyumbani.
Baada ya kufika nyumbani alipatwa na mshtuko wa moyo na kuanguka, watu wa huduma ya kwanza walifika kwenye nyumba hiyo na kuthibitisha kuwa mwanamke huyo amefariki kwa ugonjwa wa moyo.