Mh.Zitto Kabwe ametangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo lake

Mbunge wa Kigoma kaskazini Mh.Zitto Kabwe ametangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo hilo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, huku akiwashukuru wananchi wa jimbo lake kwa kumpa dhamana ya kuwawakilisha bungeni kwa kipindi cha miaka 10 licha ya kukutana na vikwazo vingi.

Akiongea na wapiga kura wake hao Zitto amesema kwa kipindi chote akiwa mbunge alijitahidi kwa kadri alivyoweza kutetea si tu maslahi kwa watu wa jimbo lake bali kwa taifa zima kwa ujumla na kwamba ataendelea kufanya hivyo kama raia ili kuondoa kila aina ya ufisadi na kutumia rasilimali za nchi kuondoa umasikini, ujinga na maradhi.
 
Baadhi ya mambo ambayo Mh.Zitto ameyataja kuwa anajisifia kuyafanya yawezekane katika jimbo lake kuwa ni pamoja na kufikisha umeme katika vijiji 16, wananchi wa jimbo lake kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, kuboresha huduma za afya, kuanzisha miradi ya bandari na soko kubwa katika kijiji cha Kagunga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo