Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Uboreshaji wa Daftari kla Kudumu
la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.Kushoto
ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na
Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama kazi ya uandikishaji wapiga kura baada ya
kuzindua Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika mji
mdogo wa Makambako Februari 24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Baadhi
ya watalaamu wa kuandikisha wapiga wakiwa na zana za kazi kabla ya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuzindua Uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda na Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa
CHADEMA John Mnyika wakitazama kadi mpya ya mpiga kura baada ya Waziri
Mkuu, kuzindua uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika
mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekititi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva (kushoto), Naibu Katibu Mkuu na Katibu
Mwenezi wa CHADEMA, John Mnyika (kulia), Yusufu Mbungiro ambaye ni Afisa
Uchaguzi na Mafunzo taifa wa Chama cha CUF (wapili kushoto) na Allan
Bujo ambaye ni Mkuu wa Ulinzi wa CHADEMA baada ya kuzindua Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako Februari
24, 2015.
Baadhi
ya watu waliohudhuria katika Uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga kura katika mji mdogo wa Makambako wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia katika uzinduzi huo Februari
24, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).