Watoto hawa wanaweza kuitwa mapacha wa miujiza baada ya kuwashangaza madaktari kutokana na kupishana kwao muda wa kuzaliwa.
Watoto hao walizaliwa katika moja ya hospitali huko Romania, sio
kwamba wametofautiana miezi miwili kuzaliwa pia wametofautiana miaka
kwani mmoja alizaliwa November 2014, mama huyo alilazimika kukaa chumba
cha kujifungulia hadi Januari 2015 ndipo akazaliwa mtoto mwingine.
Madaktari walishangazwa na hali hiyo kwa
kuwa si ya kawaida, walitegemea watoto hao wangezaliwa siku moja kama
ilivyo kawaida lakini haikuwa hivyo.
Kwa mujibu wa wataalamu walisema watoto
hao walizaliwa katika mifuko tofauti ya uzazi ambayo iliruhusu mmoja
kuzaliwa kabla ya mwenzake.