Wanawake
wa Kimasai katika kijiji cha Mabwegere wilayani Kilosa mkoani Morogoro
wamelalamikia kuishi maisha magumu baada ya wanaume kukimbia makazi na
kuwaachia mzigo wa kulea familia kufuatia mapigano yaliosababisha
mauaji ambapo wanawake wengine wamelalamikia kujifungulia majumbani
kutokana na kushindwa kumudu gharama za kwenda katika vituo vya afya.
Baadhi ya nyumba zimefungwa ambapo wakizungumza
wakiwa maporini wanawake hao wamesema baadhi ya watu wameyakimbia makazi
yao kutokana na kuishi kwa hofu ambapo wamesema migogoro hiyo ya ardhi
inawaathiri wanawake na watoto zaidi kwani wanaume wamekimbia na
kuwaachia mzigo wa kulea familia huku wengine wakikosa msaada na wengine
wakishindwa kumudu gharama za matibabu na hivyo kuomba serikali
kusimamia kumaliza migogoro hiyo.
Nae mwenyekiti wa kijiji cha Mabwegere Mika Kashu amekiri baadhi ya
wanawake kuishi katika mazingira magumu ambapo amesema waliohusika na
mauaji hayo wanafahamika na hivyo kuomba serikali iwachukulie hatua
kwani oparation ya kamatama imesababisha hofu na wanaume kulazimika
kukimbia kijiji.
Afisa utawala wa wilaya ya Kilosa Hilary Sagala akizungumza na ITV
kw anjia ya simu amesema jeshi la polisi limeimarisha ulinzi katika
eneo la Mabwegere na kuhusu wafugaji kukimbia makazi amesema hakuna
sababu ya watu kukimbia makazi kama hawakuhusika na tukio la
lililosababisha mauaji na kuwataka wananchi kurejea katika makazi yao
waendelee na shughulizao kama kawaida.