skip to main |
skip to sidebar
Vurugu Ilula Mkoani Iringa, Mwananchi afariki, Kituo cha Polisi chachomwa moto!
WANANCHI
wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, Jana wamevamia kituo cha polisi na
kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma
moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea jana asubuhi
kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na
kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye
oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.
Habari
zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara
kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha
polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la UPENDO.
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi