Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limeiagiza klabu ya simba kumlipa beki wake wa zamani Donald Mosoti jumla ya fedha taslimu dola elfu kumi na nne na mia nne ambazo ni sawa na fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 26,000,000/= ikiwa ni fidia ya kuvunja mkataba wake kinyume cha sheria .
Kwa mujibu wa taarifa zilizoko, klabu hiyo imetakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 baada ya shirikisho hilo kukubaliana na madai yake ya kuvunjiwa mkataba kinyume cha sheria .
Katika barua iliyoripotiwa kutumwa kwa klabu hiyo kupitia ofisi za shirikisho la soka nchini TFF endapo Simba itashindwa kulipa fedha hizo ndani ya muda ulioshauriwa suala hili litafikishwa kwenye kamati ya nidhamu ya Fifa kwa hatua zaidi .
Simba iliamua kuachana na beki huyu iliyemsajili toka kwenye klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya katika ya msimu uliopita huku beki huyo akilalamika mkataba wake kuvunjwa bila taratibu kufuatwa .
Beki huyo kwa sasa anachezea klabu ya Tusker ya nchini Kenya baada ya kusajiliwa akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo