Picha: Vanessa Mdee na Jux wadhihirisha mahaba mazito Afrika Kusini

Vanessa Mdee na Jux wote wapo nchini Afrika Kusini walikoenda kufanya video ambayo hata hivyo hawajasema ni ya wimbo gani na kwa mujibu wa picha wanazopost kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wanapeana kampani ya nguvu.

Hawajawahi kukubali hadharani kuwa ni wapenzi lakini picha zinaonesha wazi kuwa mastaa hao wapo kwenye dimbwi zito la mapenzi.
 
Kupromote wimbo wake mpya ‘Nikuite Nani’, Jux amepost picha akiwa na hitmaker huyo wa ‘Hawajui’ anayeonekana ‘akimchumu’ kwenye paji la uso.
 
Kabla ya picha hiyo, Jux alipost nyingine kadhaa akiwa na mrembo huyo katika pozi ambalo huwezi kuuliza kama ni marafiki tu.!

Hivi karibuni Vanessa Mdee alifunguka  kuhusu uhusiano wake na Jux na kusema: "I actually I like to keep my private life private. Nadhani kuna baadhi ya mambo ambayo hayahitaji majibu.”
 
Jux na Vanessa wameongozana na Weusi na Navy Kenzo kwenye safari hiyo ya South.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo