Baadhi
ya wakazi wa mji wa Moshi wakiashangaa lori la mafuta lilotembea bila
ya kuwa na dereva likitoka kituo cha mafuta cha Puma lilipokuwa limepaki
kwa ajili ya kushusha mafuta.tukio hilo limetokea mchana wa leo mjini
Moshi jirani na ofisi za TTCL.
Hivi
ndivyo ilivyokuwa kwa lori hilo baada ya kukata kona ya ghafla ambayo
ilisaidia madhara zaidi yasitokee baada ya tanki kukata na kurudi upande
wa barabarani na kisha kusimama.
Hata hivyo tukio hilo ambalo limewaduwaza watu wengi limesababisha uharibifu mdogo katika gari ndogo inayoonekana hapa.
Dereva
wa lori hilo ambaye jina lake halikufahamika mara moja akijaribu
kuliondoa gari hilo mara baada ya kurejea akitoka msikitini na kukuta
gari liko katikati ya barabara tofauti na sehemu alikokuwa ame paki
mwanzo.
Gari
hilo lililokuwa na mafuta ya Petrol liliondoka katika eneo hilo bila ya
tatizo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.