Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Saidi Mtanda akiwasilisha taarifa ya kamati.
Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma
SERIKALI
inatarajia kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Habari katika Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la mwezi April mwaka huu ili kujadiliwa
na kupitishwa kuwa Sheria kamili.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Saidi Mtanda
wakati akiwasilisha taarifa ya kazi za kamati yake kuanzia Januari 2014
hadi Januari 2015.
Alisema
muswada huo ni moja kati ya kilio cha wadau wa habari nchini ambao
unatarajiwa kuikomboa taaluma hiyo kwa kusimamia masuala yote yanayohusu
taaluma hiyo muhimu duniani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akijibu swali Bungeni.
Akizungumzia
huhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake, Mwenyekiti Mtanda
alipendekeza kuwa halmashauri zote nchini ambazo hazijatenga asilimia 5
ya wanawake na asilimia 5 ya vijana ziorodheshwe na zichukuliwe hatua
kali.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizopo, tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Mandeleo ya
Vijana na Wanawake mwaka 1993, ni halamashauri chache zimekuwa zikitenga
fedha hizo kama inavyotakiwa.
Katika
taarifa yake, Mwenyekiti Mtanda alionesha kuridhishwa na maendeleo ya
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa halamashauri ya Wilaya ya Temeke ulio
chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Alisema
katika ziara ya kutembelea mfuko huo Januari 19 mwaka huu, walitembelea
miradi ya vijana ya kikundi cha Sokoine Youth Development, Waungwana
Youth Family na African Legends.
Kwa
upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, Mwenyekiti alizipongeza
halmashauri ya mji Korogwe na zingine ambazo zimekuwa mfano wa kuigwa
kwa kutenga fedha za mfuko huo na kuzitumia kama ilivyokusudiwa.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela.
Mbali
na mradi huo, alisema kamati pia ilitembelea mradi wa vituo vya
kurushia matangazo ya Redio Mafifi, Iringa na Kola Hill, Morogoro
uliogharimu shilingi Milioni 200.
“Mradi
wa Mafifi Gangilonga, Iringa ni katika ya miradi mikubwa ya kufunga
mitambo ya kurushgia matangazo katika vituo 9…Maeneo yaliyonufaika na
mradi huu ni mkoa wa Manyara, Morogoro, Moshi, Mpanda, Newala,
Shinyanga, Songea na Tunduru” alisema Mtanda.
Alisema
mradi huo umewezesha kupatikana kwa matangazo ya redio kwa ubora zaidi
ambapo matangazo hayo yanapatikana katika masafa ya FM-TBC Taifa
(107.1MHz) na TBC FM (96.2MHz).
Aliongeza
kuwa mradi huo umeweza kuongeza usikivu wa matangazo ya Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) kwani kwa sasa yanasikika katika maeneo mengi
zaidi nje ya mji wa Iringa.
Mwenyekiti Mpya wa Bunge, Kidawa Salehe akiongoza Bunge.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Margareth Sitta akiwasilisha taarifa ya kamati yake.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Vicky Kamata akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Bungeni.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Susan Lyimo akiuliza swali kwa Waziri Mkuu.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Al- Shaymaa Kwegyir akichangia taarifa ya kamati.
Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba akichangia taarifa ya kamati.
Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia kikao cha Bunge.
Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu (kulia) akiambatana na wenzake kutoka nje ya ukumbi wa Bunge,huku wakibadilishana mawazo.
Mbunge
wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, akimpa mkono Mwenyekiti Mpya
wa Bunge Kidawa Saleh, kumpongeza kwa kuliongoza Bunge huku Mwenyekiti
mpya mwenzake Lediana Mng’ong’o (kushoto) na mbunge Martha Mlata
wakifumrahia.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kushoto)akiteta jambo na
Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi.(Picha zote na Hussein
Makame-MAELEZO,Dodoma).